Zambia yaandaa mkutano kuhusu uzoefu wa China katika maendeleo ya nishati mbadala

(CRI Online) Desemba 04, 2024

Mkutano kuhusu uzoefu wa China katika maendeleo ya nishati mbadala umefanyika nchini Zambia ikiwa ni sehemu ya juhudi za kusaidia Bara la Afrika kuleta mchanganyiko wa nishati mbalimbali.

Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Umeme cha Shanghai kwa ushirikiano na Taasisi ya Taifa ya Uongozi wa Umma ya Zambia (NIPA) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Nishati na Ushirikiano Duniani (GEIDCO).

Mkutano huo umewaleta pamoja wataalamu, watendaji wa sekta na watunga sera, ili kubadilishana uzoefu kuhusu maendeleo ya nishati mbadala, ukiwa na washiriki kutoka Kenya, Nigeria, na Afrika Kusini.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Umeme cha Shanghai Bw. Gu Chunhua, amesema mkutano huo ulikuwa na lengo la kutumia utaalamu wa chuo kikuu hicho katika nishati mbadala na kuchangia mafanikio ya China na utafiti wa kiufundi katika nishati mbadala pamoja na vyuo vikuu vya Zambia na kampuni za umeme.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha