China inashikilia dhamira yake ya kufungua mlango kwenye ngazi ya juu: Waziri wa Mambo ya Nje wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 05, 2024
China inashikilia dhamira yake ya kufungua mlango kwenye ngazi ya juu: Waziri wa Mambo ya Nje wa China
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitazama onyesho pamoja na wageni katika shughuli ya kutangaza Bandari ya Biashara Huria ya Hainan iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya China mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 4, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

BEIJING - China ina dhamira ya maendeleo kupitia ufunguaji mlango wa ngazi ya juu na itaendelea kuhimiza mazingira ya biashara ambayo yana patikana masoko, kufuata sheria na kuwa ya kimataifa, kuhimiza ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kutekeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi amesema mjini Beijing siku ya Jumatano.

Wang amesema hayo katika shughuli ya kutangaza Bandari ya Biashara Huria ya Hainan kwa dunia iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya China mjini Beijing, mji mkuu wa China.

Maofisa wakuu wa mkoa wa Hainan wa China walialikwa kutoa maelezo kwa watu zaidi ya 500 waliohudhuria, wakiwemo wanadiplomasia na maofisa kutoka nchi zaidi ya 160, wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa, maofisa wa serikali kuu na serikali za mitaa, na wawakilishi kutoka kampuni, jumuiya za wafanyabiashara za kimataifa na vyombo vya habari vya ndani na nje ya China.

Mwezi Juni, 2020, China ilitoa mpango wa jumla wenye malengo ya kujenga kisiwa kizima cha Hainan kuwa bandari ya biashara huria yenye ushawishi mkubwa duniani na ya kiwango cha juu kufikia katikati ya karne hii.

Wang amesema kuwa ujenzi wa bandari hiyo ya biashara huria ya Hainan umeshika kasi na eneo hilo limevutia idadi inayoongezeka ya kampuni za kikanda na kimataifa kuwekeza na kuendesha biashara, ikionyesha mazingira mapya na yenye hamasa ya uwazi na maendeleo.

Bandari ya Biashara Huria ya Hainan imekuwa mstari wa mbele mpya wa kufungua mlango wa utaratibu wa China, sehemu mpya ya ushirikiano wa kunufaishana kikanda, na injini mpya inayoendesha utandawazi wa kiuchumi, Wang amesema.

"Kuona ni kuamini, na kila mtu anakaribishwa kutembelea Hainan na kujionea hali halisi kwa macho yake," ameongeza.

Wang amesema China itaendelea na njia yake ya kujiendeleza kwa kufungua mlango, yenye uvumbuzi, kijani, jumuishi na ya amani.

"Kuichagua China kunamaanisha kuchagua fursa, na kuikumbatia China kunamaanisha kukumbatia siku za baadaye," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha