

Lugha Nyingine
Kenya kuendelea na ushirikiano wa kimkakati wa muda mrefu na China
Kenya imesema itaendelea kuhimiza ushirikiano mzuri na wa muda mrefu na China pamoja na kulinda maslahi ya Wachina wanaoishi nchini humo.
Akiongea kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa China nchini Kenya anayemaliza muda wake, Bw. Zhou Pingjian, mkuu wa mawaziri ambaye pia ni Waziri wa Masuala ya Kigeni na Diaspora wa Kenya, Bw. Musalia Mudavadi amesema uhusiano kati ya Kenya na China utaimarishwa zaidi ili kufikia ushirikiano wa pande zote wa kimkakati, na wenye kuleta manufaa kwa pande zote na unaozingatia maslahi ya watu.
Bw. Mudavadi pia amesema serikali ya Kenya itahakikisha kuwa jamii ya Wachina, ambayo imeisaidia serikali ya Kenya kufikia vipaumbele vya maendeleo ya kitaifa, iko salama na uwekezaji wao.
Ameongeza kuwa ushirikiano huo ambao umekuwepo kwa miongo kadhaa, umekuwa ni msingi wa maono ya pamoja ya kujenga jumuiya ya karibu yenye mustakabali wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma