

Lugha Nyingine
Zanzibar yapata dola za kimarekani milioni 3.4 kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya kihistoria ya Mji Mkongwe
Rais Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar ya Tanzania ametangaza Jumanne kuwa Zanzibar imepata dola za kimarekani milioni 3.4 kwa ajili ya ukarabati wa majengo wa kihistoria katika Mji Mkongwe.
Rais Mwinyi ametangaza hilo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mji Mkongwe katika eneo la Forodhani, visiwani humo.
Rais Mwinyi amesema fedha hizo zilizotolewa na kampuni ya uendelezaji wa mali isiyohamishika ya Infinity Group yenye makao makuu Dubai, Falme za Kiarabu, zitatumika kujenga upya majengo yaliyoharibika ndani ya Mji Mkongwe.
Pia ameongeza kuwa serikali inatafuta fedha zaidi kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuhakikisha inaboresha majengo ya Mji Mkongwe yenye umri wa zaidi ya miaka 194.
Amewataka wakazi wa Mji Mkongwe kuendelea kuuhifadhi mji huo, ili kuhakikisha unahifadhiwa kwa miaka 100 ijayo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma