

Lugha Nyingine
Jukwaa la Mji wa Sayansi wa Guangming 2024 lafunguliwa
Picha ikionyesha hafla ya kuzinduliwa kwa miundombinu muhimu kwenye Jukwaa la Mji wa Sayansi wa Guangming. (Picha na waandalizi wa jukwaa)
Jukwaa la Mji wa Sayansi wa Guangming 2024 limefunguliwa katika Eneo la Guangming la Mji wa Shenzhen, China siku ya Alhamisi, Tarehe 5, Desemba, na mafanikio mbalimbali ya kivumbuzi na sera zimetangazwa kwa umma.
Jukwaa hilo limepangwa kufanyika kwa siku mbili za Alhamisi na leo Ijumaa, likijumuisha hafla ya ufunguzi, mkutano wa washiriki wote, majukwaa saba madogo na shughuli ya matembezi na mawasiliano.
Kwenye jukwaa hilo, miundombinu mingi muhimu ya kisanyansi na kiteknolojia na taasisi za utafiti wa kisayansi zimetoa mwaliko wa pamoja kwa taasisi za utafiti wa kisayansi, kampuni za kisanyansi na kiteknolojia na wadau wa sayansi na teknolojia duniani kote, ili kuimarisha mabadilishano na ushirikiano wa kimataifa wa sayansi na teknolojia, na kuhimiza kwa pamoja uvumbuzi kutoka mwanzo.
Jukwaa hilo limeandaliwa na serikali Mji wa Shenzhen, na kuungwa mkono na Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong. Mji wa Sayansi wa Guangming, ambao jukwaa hilo limejikita kwake, ni sehemu tangulizi ya kielelezo ya Kituo Jumuishi cha Kitaifa cha Sayansi cha China cha Eneo la Ghuba Kubwa ya Guangdong-Hong Kong-Macao.
Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Shenzhen umeshikilia lengo la kujenga “Mji Bora wa Sayansi Duniani” ili kuhudumia mkakati wa China wa kujitegemea na kujiimarisha katika sayansi na teknolojia, na umetumia nguvu za kifursa za mji huo kuhimiza ujenzi wa Mji wa Sayansi wa Guangming.
Picha ikionyesha hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la Mji wa Sayansi wa Guangming. (Picha na waandalizi wa jukwaa)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma