Mji Mkuu wa Syria, Damascus waangukia mikononi mwa waasi huku Rais al-Assad akikimbia Syria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2024

Wakazi wa Damascus, Syria wakifanya mkutano wa hadhara mtaani humo  Desemba 8, 2024. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)

Wakazi wa Damascus, Syria wakifanya mkutano wa hadhara mtaani humo Desemba 8, 2024. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)

DAMASCUS - Vikosi vya makundi ya upinzani yenye silaha vimedhibiti kikamilifu Damascus, mji mkuu wa Syria jana Jumapili, vikikomesha utawala wa familia ya Assad wa zaidi ya miongo mitano, ambapo serikali ya Rais Bashar al-Assad imeanguka kwa kasi baada ya kukumbwa na mashambulizi makali ya waasi yasiyofikia wiki mbili. Operesheni hiyo imefikia kilele chake baada ya waasi hao kutangaza kwamba Assad ameukimbia mji mkuu na kuachia madaraka.

Baadaye mchana, vyombo vya habari vya serikali ya Russia vilitangaza kwamba Assad amefika Moscow, na amepewa hifadhi pamoja na familia yake.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa taarifa ikisema kuwa Assad "ameamua kuacha wadhifa wa urais na kuondoka nchini humo, akitoa agizo la kukabidhi madaraka kwa amani."

Rais wa Syria Bashar al-Assad akihudhuria Mkutano Maalum wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na za Kiislamu mjini Riyadh, Saudi Arabia, Novemba 11, 2024. (SPA kupitia Xinhua)

Rais wa Syria Bashar al-Assad akihudhuria Mkutano Maalum wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na za Kiislamu mjini Riyadh, Saudi Arabia, Novemba 11, 2024. (SPA kupitia Xinhua)

Nchini Syria, mkuu wa Hayat Tahrir al-Sham (HTS) Abu Mohammad Al-Jolani, aliyeongoza mashambulizi hayo ya radi, amesema Mohammad Ghazi Al-Jallali, aliyeteuliwa kuwa waziri mkuu na al-Assad mwezi Septemba, atasimamia kwa muda vitengo vya kiumma.

Al-Jolani ameviagiza vikosi vya makundi ya upinzani mjini Damascus kuacha kukaribia vitengo vya kiumma na kupiga marufuku usherehekeaji wa kufyatu risasi.

Waziri mkuu Al-Jallali pia ametoa wito wa kuwataka Wasyria kulinda vituo vya kiumma, akisema vituo hivyo ni vya raia wote.

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha mwonekano wa jiji la Damascus, Syria, Desemba 8, 2024. (Picha na Monsef Memari/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha mwonekano wa jiji la Damascus, Syria, Desemba 8, 2024. (Picha na Monsef Memari/Xinhua)

Hata hivyo, matukio mawili yaliyorikodiwa yalionesha uporaji wa watu wengi waliovamia nyumba ya Assad na ikulu mbili za rais.

Katikati ya msukosuko huo, Israel imefanya mfululizo wa upigaji mabomu kutoka angani usioonekana hapo kabla, ukishambulia maeneo ya zamani ya usalama na kijeshi ya Syria mjini Damascus na Quneitra mara kwa mara ndani ya siku moja, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Baadhi ya mashambulizi hayo ya Israel yalilenga vituo na majengo ya jeshi yaliyoachwa hapo awali karibu na Damascus. Vikosi vya ardhini vya Israel pia vimeripotiwa kusonga mbele katika sehemu za Jabal al-Sheikh, vikichukua udhibiti wa vituo vya zamani vya usimamizi katika hali isiyo na upingaji.

Wakati huo huo, Muungano wa Kitaifa wa Syria, ambao ni muungano wa makundi ya upinzani yaliyoanzishwa uhamishoni kufuatia uasi wa mwaka 2011 dhidi ya Assad, umeapa siku hiyo ya Jumapili kuendelea kufanya juhudi za kukabidhi mamlaka kwa chombo cha usimamizi wa mpito chenye mamlaka kamili ya mambo ya utawala, kwa lengo la kukaribisha nchi ya Syria yenye uhuru, demokrasia, na vyama vingi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha