

Lugha Nyingine
Makamu wa Rais wa Ghana Bawumia akubali kushindwa katika uchaguzi wa urais
Mpiga kura akipiga kura katika kituo cha kupigia kura mjini Accra, Ghana, Desemba 7, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)
ACCRA - Makamu wa Rais wa Ghana ambaye pia ni mgombea wa urais wa chama tawala cha New Patriotic, Mahamudu Bawumia amekubali kushindwa mapema jana Jumapili katika uchaguzi wa urais wa Mwaka 2024 uliofanyika Jumamosi nchini Ghana.
Katika hotuba yake fupi kwa njia ya televisheni kutoka kwenye makazi yake rasmi, Bawumia amekubali matokeo ya uchaguzi huo, akitoa shukrani kwa Waghana kwa uungaji mkono wao, na kutoa pongezi kwa Rais wa zamani John Dramani Mahama kwa ushindi wake katika kinyang'anyiro cha urais.
Mahama, ambaye anaongoza chama cha upinzani cha National Democratic Congress, ametangaza ushindi wake siku ya Jumapili kwenye mitandao ya kijamii. Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X (jina lake la awali ni Twittrer) Mahama ameeleza kuwa ushindi wake ni "ushindi mkubwa" na kusema kuwa amepokea simu ya pongezi kutoka kwa Bawumia.
Raia wa Ghana walipiga kura zao kwenye uchaguzi huo wa rais mpya na wabunge 276 uliofanyika Jumamosi iliyopita.
Tume ya Uchaguzi ya Ghana bado haijatangaza rasmi matokeo ya mwisho.
Wafanyakazi wakihesabu kura katika kituo cha kupigia kura mjini Accra, Ghana, Desemba 7, 2024. (Xinhua/Seth)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma