

Lugha Nyingine
Vijana wa Kenya wahitimu mafunzo ya kuboresha ujuzi wa kidijitali yanayofadhiliwa na Huawei
Vijana wanateknolojia zaidi ya 100 wa Kenya wamehitimu mafunzo yaliyofadhiliwa na kampuni kubwa ya teknolojia ya China, Huawei yenye lengo la kuboresha ujuzi wao wa kidijitali, yakiwaandaa kwa ajili ya jukumu muhimu nchini humo la kujikita kwenye uchumi unaotegemea maarifa.
Mahafali ya kuhitimu mafunzo hayo, yamefanyika Jumamosi mjini Nairobi, yakiashiria kukamilika kwa mafanikio kwa mafunzo hayo ya Huawei DigiTruck yaliyohusisha vijana 180. Hafla ya mahafali hayo ilihudhuriwa na wabunge, viongozi wa kijamii, watendaji wa biashara, na wabunifu.
Mkurugenzi wa vyombo vya habari wa Huawei Tawi la Kenya, Khadija Mohammed Ahmed, amesema kuwa wahitimu hao siyo tu wamepata ujuzi wa hali ya juu wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) bali pia wameonesha ari ya kutoa mchango kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa kidijitali wa Kenya.
DigiTruck iliyozinduliwa mwaka 2019 chini ya mpango wa Huawei wa TECH4ALL, ni darasa linalohama, likitumia nishati ya jua na kuwekewa intaneti, laptop na simu janja. Linasafiri na kufika kwenye jamii za mbali, likitoa mafunzo bila malipo ya TEHAMA kwa vijana kote nchini Kenya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma