

Lugha Nyingine
Uongozi wa Juu wa CPC wafanya mkutano kuhusu kazi ya uchumi ya Mwaka 2025, ujenzi wa mienendo na maadili ya Chama na mapambano dhidi ya ufisadi
BEIJING - Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano jana Jumatatu wa kuchambua na kujadili kazi ya uchumi ya Mwaka 2025 na kupanga ujenzi wa mienendo na maadili ya Chama na mapambano dhidi ya ufisadi, ambapo mkutano huo umeongozwa na Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya chama hicho ambaye pia ni Rais wa China.
Mkutano huo umesema kuwa, mwaka huu ni muhimu kwa kufikia malengo na majukumu yaliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa 14 wa Miaka Mitano wa China (2021-2025), na uendeshaji uchumi umekuwa shwari kwa ujumla huku hatua zikipigwa, ambapo nguvu ya kiuchumi, uwezo wa kisayansi na kiteknolojia, na nguvu ya jumla ya nchi zimeendelea kuimarishwa.
Malengo na majukumu makuu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Mwaka 2024 yatatimizwa kwa mafanikio, umesema mkutano huo na kwamba kwa ufanisi mzuri wa kiuchumi wa Mwaka 2025, ni lazima kuchukua sera za jumla zinazohimiza juhudi zaidi na kuleta nguvu ya uhamasishaji zaidi.
Mkutano huo umehimiza kutekeleza sera ya kibajeti zinazohimiza juhudi zaidi na sera ya mambo ya fedha yenye kulegeza kiasi.
Mkutano huo umesema, ni muhimu kuongeza na kukamilisha zana za sera, kuimarisha marekebisho ya kuepusha na kukabiliana na mdororo usio wa kawaida, kuimarisha uratibu wa sera mbalimbali, na kufanya marekebisho na udhibiti wa uchumi mkuu kuwa wenye kutazama mbele zaidi, kulenga malengo na wenye ufanisi zaidi.
Nchi ya China inapaswa kuongeza nguvu ya kuhimiza matumizi katika manunuzi, kuinua ufanisi wa uwekezaji, na kupanua mahitaji ya ndani katika mambo yote, mkutano umesema.
Mkutano huo umesisitiza kustawisha nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora zinazotegemea uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, kuendeleza ujenzi wa mfumo wa viwanda vya mambo ya kisasa, kuwezesha mageuzi ya mfumo wa kiuchumi yafanye kazi ya uelekezaji, na kuhakikisha hatua za mageuzi ya kielelezo zinatekelezwa kwa ufanisi.
Nchi inapaswa kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu na kuleta utulivu kwenye biashara na nje na uwekezaji, vilevile kuzuia na kupunguza hatari kwa ufanisi katika sekta muhimu ili kuhakikisha hakuna hatari za kimfumo zinazotokea, mkutano huo umeeleza.
Kabla ya mkutano huo, Xi aliongoza mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, ambao ulisikiliza ripoti za kazi za Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI) na Kamati ya Ukaguzi ya Kitaifa Mwaka 2024.
Mkutano huo umekubali kuwa, mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu utafanyika kuanzia Januari 6 hadi 8, 2025.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma