China yaeleza matumaini ya Syria kupata suluhu ya kisiasa haraka iwezekanavyo kwa ajili ya maslahi ya Wasyria

(CRI Online) Desemba 10, 2024

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning amesema China inatumai pande zote zinazohusika zitatafuta suluhu ya kisiasa ili kurejesha utulivu haraka iwezekanavyo kwa kuzingatia kanuni ya kuwajibika kwa maslahi ya muda mrefu na kuzingatia maslahi ya kimsingi ya watu.

Bi. Mao ameyasema hayo wakati akijibu maswali husika kuhusu hali ya Syria ambapo ameongeza kuwa China inatilia maanani sana hali ya Syria, na kwamba mustakabali na hatma ya Syria inapaswa kuamuliwa na Wasyria.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha