Rais wa Botswana akutana na ofisa mwandamizi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 10, 2024

GABORONE - Rais wa Botswana Duma Boko amekutana na Shao Hong, naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) huko Gaborone, mji mkuu wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Shao kwanza amewasilisha salamu za kikunjufu za Rais Xi Jinping wa China kwa Duma Boko, akisema kuwa China inatilia maanani sana uhusiano wa China na Botswana, inaunga mkono mipango ya utawala ya serikali mpya, kuenzi urafiki wa jadi, na kutumia kikamilifu nguvu ya ushirikiano.

Shao amesema kuwa, China inapenda kushirikiana na Botswana katika kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, kuhimiza kwa pamoja ujenzi wa mambo ya kisasa, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya kujenga jumuiya ya siku zote ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

Shao pia ameelezea misingi ya Mkutano wa Tatu wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China.

Kwa upande wake, Rais Boko amemuomba Shao kuwasilisha salamu zake za dhati na salamu za kutakia kila keri kwa Rais Xi, akisema kuwa China ilituma ujumbe wa ngazi ya juu nchini Botswana muda mfupi baada ya serikali mpya kuingia madarakani, ikionyesha uungaji mkono wa kithabiti wa China kwa Botswana.

Amesisitiza kwamba nchi yake inashikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na kueleza nia yake ya kuimarisha ushirikiano na China wa kufuata hali halisi katika sekta mbalimbali, kuendeleza urafiki wa jadi, na kusukuma uhusiano wa pande mbili kuendelezwa kwenye ngazi ya juu zaidi.

Katika ziara hiyo nchini Botswana, Shao na ujumbe wake wa Kamati ya Kitaifa ya CPPCC pia walikutana na Spika wa Bunge la Botswana na maofisa wengine. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha