

Lugha Nyingine
Tanzania yatangaza mgombea mpya wa nafasi ya ukurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika
(CRI Online) Desemba 11, 2024
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania Jumanne ametangaza kuwa Tanzania itamteua Mohamed Janabi kuwa mgombea wa nafasi ya ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika.
Janabi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mshauri wa rais wa masuala ya afya na tiba atachukua nafasi ya mkurugenzi mteule wa WHO Kanda ya Afrika marehemu Faustine Ndugulile, ambaye alifariki tarehe 7 Novemba wakati akipatiwa matibabu nchini India.
Ndugulile aliteuliwa katika Mkutano Mkuu wa 74 wa WHO uliofanyika Agosti mwaka 2024 mjini Brazzaville, Jamhuri ya Congo, na alikuwa akitarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi Machi mwaka 2025.
Rais Samia amesema ana imani juu ya sifa na uzoefu mkubwa wa Janabi kwenye sekta ya afya.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma