Ethiopia yatarajia kuuza kahawa zaidi nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 11, 2024

Picha hii ikionyesha wafanyakazi wakichambua maharagwe ya kahawa yaliyokaangwa katika kiwanda cha kukaanga kahawa mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, tarehe 8 Juni 2024. (Xinhua/Liu Fangqiang)

Picha hii ikionyesha wafanyakazi wakichambua maharagwe ya kahawa yaliyokaangwa katika kiwanda cha kukaanga kahawa mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, tarehe 8 Juni 2024. (Xinhua/Liu Fangqiang)

ADDIS ABABA - Serikali ya Ethiopia imeonyesha nia ya kupenyeza zaidi kwenye soko la kahawa la China linalokua kwa kasi huku China ikiwa moja ya nchi zinazoongoza kwa mauzo ya nje ya kahawa ya Ethiopia.

Wito huo umetolewa na maafisa wa Mamlaka ya Kahawa na Chai ya Ethiopia (ECTA) kwenye majadiliano na wawakilishi wa wafanyabiashara wa China ambao wana nia ya kununua kahawa ya nchi hiyo, ECTA imesema katika taarifa iliyotolewa Jumatatu.

Kwenye majadiliano hayo, maafisa wa ECTA na wauzaji nje kahawa wa Ethiopia wamesisitiza umuhimu wa kukua kwa soko la China kwa wauzaji kahawa wa Ethiopia, huku China ikiwa miongoni mwa waagizaji nje 10 wakubwa wa kahawa ya Ethiopia.

Huku kukiwa na ongezeko la kasi la mauzo ya nje ya kahawa ya Ethiopia nchini China katika miaka ya hivi karibuni, maafisa na wauzaji nje hao wa kahawa wamesema ongezeko la idadi ya watumiaji wa kahawa na kupendwa kwa kahawa ya Ethiopia miongoni mwa wachina kunahimiza soko la nje la kahawa la Ethiopia.

Picha hii iliyopigwa tarehe 1 Julai 2023 ikionyesha maharagwe ya kahawa katika Kampuni ya Mullege Public, kampuni ya familia ya usindikaji na uuzaji nje wa kahawa ya Ethiopia, mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

Takwimu zinaonyesha kuwa, katika miaka mitatu hivi iliyopita, kiasi cha kahawa inayouzwa ya Ethiopia nchini China kimekuwa kikiongezeka kwa wastani wa asilimia 27 kwa mwaka, hali ambayo inatokana na ongezeko kubwa la wanunuzi wa kahawa kutoka China wanaoagiza kahawa nje moja kwa moja kutoka Ethiopia.

Ethiopia, inayosifika kwa uzalishaji wake wa kahawa, ilipata dola za Kimarekani bilioni 1.43 kutokana na mauzo ya nje ya kahawa katika mwaka uliopita wa fedha wa Ethiopia, uliomalizika Julai 7, 2024. Taifa hilo la Afrika Mashariki linalenga kuongeza kiasi hicho hadi kufikia dola za Kimarekani bilioni 2 katika mwaka wa sasa wa fedha wa 2024/2025.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha