

Lugha Nyingine
Vikwazo vya Marekani vinalenga kuzuia haki ya kujiendeleza ya watu wa China
BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema Jumatano kuwa, vikwazo vya hivi karibuni ambavyo Marekani imeweka dhidi ya kampuni za teknolojia ya hali ya juu za China ni jaribio la wazi la kukandamiza kampuni hizo kwa kisingizio cha haki za binadamu, akidhihirisha kuwa hatua hiyo imefichua tena kusudi halisi la Marekani la kuzuia haki ya kujiendeleza ya watu wa China.
Msemaji Mao amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati akijibu swali kuhusu Wizara ya Biashara ya Marekani kuongeza majina ya kampuni mbili za teknolojia ya hali ya juu za China kwenye "Orodha ya Vikwazo" kwa ati sababu ya "kukiuka haki za binadamu."
"Kulinda haki za binadamu ni kisingizio tu wanachotumia kufikia lengo lao. Mpango kama huo hautaweza kufanikiwa," Msemaji Mao amesema.
Ameeleza kuwa kama Marekani inafuatilia kweli hali ya haki za binadamu, inapaswa kushughulikia kwanza nakisi yake ya haki za binadamu, badala ya kuyafanya masuala ya haki za binadamu yawe ya kisiasa na kuyatumia kama silaha ili kudhuru maslahi ya nchi nyingine na kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma