Marufu ya kutotoka nje mjini Damascus yaondolewa huku Waziri Mkuu wa muda akitoa wito kwa wakimbizi kurejea nyumbani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 12, 2024

Watu wakitembea kwenye mtaa mjini Damascus, Syria, Desemba 10, 2024. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)

Watu wakitembea kwenye mtaa mjini Damascus, Syria, Desemba 10, 2024. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)

DAMASCUS - Mamlaka ya Operesheni za Kijeshi ya Syria imetangaza jana Jumatano kuondolewa kwa marufuku ya kutotoka nje mjini Damascus na maeneo jirani, ukiwataka wakaazi kurejea kazini wakati nchi hiyo ikikabiliana na athari za kupinduliwa kwa Bashar al-Assad ambapo tangazo hilo limeenda sambamba na Waziri Mkuu wa muda Mohammed al-Bashir kutoa wito kwa wakimbizi kurejea nyumbani.

Al-Bashir, kiongozi wa zamani wa eneo la kaskazini-magharibi mwa Syria, aliteuliwa Jumanne kuongoza serikali ya mpito hadi Machi 2025. Uteuzi huo unafuatia mashambulizi ya haraka ya muungano wa wanamgambo unaoongozwa na Hayat Tahrir al-Sham (HTS), ambao umeishikilia Damascus ndani ya siku 12 baada ya kuanzisha mashambulizi yake kutoka kaskazini mwa Syria Novemba 27. Assad ameikimbia nchi, ikihitimisha miongo mitano ya utawala wa familia yake.

Picha hii iliyopigwa Desemba 8, 2024 ikionyesha wapiganaji waasi mjini Damascus, Syria. (Str/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Desemba 8, 2024 ikionyesha wapiganaji waasi mjini Damascus, Syria. (Str/Xinhua)

Uongozi huo mpya, unaotawaliwa na wapiganaji wa Kiislamu wa HTS, umejaribu kuwahakikishia watu wa madini madogo na kuahidi kwamba haki za makundi yote ya kidini na kikabila zitahakikishwa.

Wakati huo huo, kiongozi wa HTS Abu Mohammed al-Jolani ameahidi haki kwa "waathirika" wa utawala wa Assad, akisema kuwa maafisa katika serikali ya Assad waliohusika katika mateso hawatasamehewa.

Katika sehemu ya kaskazini-mashariki, vikosi vinavyoongozwa na Wakurdi vimetangaza usimamishaji vita uliosuluhishwa na Marekani siku hiyo ya Jumatano na wanamgambo wanaoungwa mkono na Uturuki katika mji wa kimkakati wa Manbij. Siku za mapigano makali katika mji huo wenye Waarabu wengi zilizuka baada ya vikosi vinavyoongozwa na HTS kuiangusha serikali ya Assad siku ya Jumapili.

Vikosi vya Kidemokrasia vya Syria (SDF), muungano wa wanamgambo unaoongozwa na Wakurdi unaoungwa mkono na Marekani, vimeripoti kwamba wapiganaji 218 wameuawa katika mapigano hayo na kuahidi kujiondoa katika eneo hilo "haraka iwezekanavyo."

Kamandi Kuu ya Marekani ilithibitisha Jumanne kwamba mkuu wake, Jenerali Michael Kurilla, alikuwa ametembelea kambi za kijeshi za Marekani nchini Syria na kukutana na washirika wa SDF.

Mtu akijipiga picha ya selfie mjini Damascus, Syria, Des. 10, 2024. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)

Mtu akijipiga picha ya selfie mjini Damascus, Syria, Des. 10, 2024. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)

Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei amesemakuondolewa kwa Assad hakujapunguza ushawishi wa Tehran kikanda, akipuuza maneno kwamba kudhoofika kwa mchango wa Syria katika "upinzani" dhidi ya Israeli kutapunguza nguvu ya Iran.

Khamenei ameishutumu Marekani, Israel, na "nchi jirani" ambayo hakuitaja jina kwa kupanga mapinduzi dhidi ya Assad.

Qatar imetangaza mipango ya kufungua tena ubalozi wake mjini Damascus, ikirejelea uhusiano wa kihistoria na dhamira ya kuunga mkono ukarabati wa Syria.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha