Baraza Kuu la UN lapitisha azimio la kusimamishwa mapigano mara moja katika Ukanda wa Gaza

(CRI Online) Desemba 12, 2024

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limefanya kikao maalum cha dharura na kupitisha kwa kura nyingi azimio lisilo na vifungu vya kutekelezwa kisheria na pande husika la kutaka usimamishaji mapigano wa mara moja, usio na masharti na wa kudumu katika Ukanda wa Gaza.

Azimio hilo limepitishwa kwa kura 158 za ndiyo, kura 9 za hapana, na 13 za kujizuia. Marekani na Israel zimepiga kura ya hapana. Azimio hilo lililowasilishwa na Indonesia pia limetaka kuachiliwa mara moja kwa watu wote wanaoshikiliwa mateka.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na idara ya afya ya Gaza, tangu duru mpya ya mgogoro huo kati ya Palestina na Israel ilipoanza mwezi Oktoba mwaka jana, operesheni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza zimesababisha vifo vya Wapalestina karibu elfu 45 huku watu zaidi ya laki moja na elfu sita wakijeruhiwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha