

Lugha Nyingine
Mradi unaofadhiliwa na China kwa ajili ya kuwezesha vijana wa Afrika waangaziwa katika kongamano nchini Kenya
Wajumbe wa Jukwaa la 2024 la UNESCO kuhusu Elimu ya Juu Barani Afrika lililofanyika Nairobi, Kenya wamesema Jumatano kuwa mradi unaofadhililiwa na fedha kutoka China “Funds-in-Trust” Awamu ya 3 (CFIT III), ulioanzishwa na serikali ya China kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), umekuwa na mchango kimageuzi katika kuwawezesha vijana wa Afrika kupata ujuzi ulio mwafaka kwa soko.
Ukiwa ulizinduliwa mwaka 2019, mradi wa Awamu ya 3 (CFIT III) umeshazinduliwa katika nchi sita za Afrika kuongeza uwezo wa taasisi za elimu ya juu ili kuwapa vijana wenyeji ujuzi wa kiufundi na wa msingi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira.
Mafanikio ya mradi huo yaliangaziwa katika jukwaa hilo lililoandaliwa kwa pamoja na UNESCO, Umoja wa Afrika (AU), na serikali ya Kenya na kufanyika Jumanne na Jumatano.
Balozi wa China kwenye UNESCO Yang Xinyu amesisitiza jukumu muhimu la elimu katika uhusiano kati ya China na Afrika, akiongeza kuwa tangu kuanzishwa kwake, mradi huo wa awamu ya 3 ya CFIT umeongeza uwezo wa taasisi za elimu ya juu za Afrika kushughulikia mahitaji yanayoongezeka ya wafanyakazi wenye ujuzi katika sekta muhimu za kiuchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma