China yasema hakuna mshindi kwenye vita ya biashara inayoharibu minyororo ya viwanda na usambazaji bidhaa ya kimataifa

(CRI Online) Desemba 13, 2024

Rais Xi Jingping wa China hivi karibuni alipokutana na wakurugenzi wa mashirika ya kiuchumi ya kimataifa amefafanua msimamo thabiti wa China kuhusu maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani, akisisitiza kuwa hakuna mshindi kwenye vita ya ushuru, biashara, sayansi na teknolojia inayoenda kinyume na mkondo wa kihistoria na kanuni za kiuchumi.

Kwenye mazungumzo yao, wakurugenzi wa mashirika ya kiuchumi ya kimataifa wamesema kuwa China siku zote ni injini muhimu na nanga ya utulivu kwa ukuaji wa uchumi wa dunia.

Wamesema, China pia ni mtetezi thabiti wa mifumo ya pande nyingi, na kwamba mashirika hayo yanapenda kuimarisha ushirikiano na uratibu na China, ili kulinda biashara huria na utandawazi wa kiuchumi.

Wamesema kuwa inakubalika kimataifa kuwa China imetoa ishara bayana ya kufungua mlango na kupanua ushirikiano, hatua ambayo imeinua imani ya pande zote katika kulinda utulivu wa minyororo ya viwanda na usambazaji bidhaa ya kimataifa.

Wakati dunia ya leo inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimataifa, jumuiya ya kimataifa inatarajia kuwa uhusiano kati ya China na Marekani utaelekea kwenye mwelekeo wenye utulivu na uendelevu, na kutoa mchango zaidi katika kutuliza minyororo ya viwanda na usambazaji bidhaa.

China na Marekani zikiwa ni sehemu mbili muhimu za minyororo hiyo, ni kwa kupitia mawasiliano na ushirikiano, ndipo zitanufaisha dunia nzima.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha