

Lugha Nyingine
Umoja wa Afrika wakaribisha makubaliano kati ya Ethiopia na Somalia kuhusu mzozo wa Somaliland
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat amekaribisha makubaliano ya hivi karibuni yaliyosainiwa na viongozi wa Ethiopia na Somalia kuhusu mgogoro wa Somaliland, eneo lililojitangaza kujitenga la Somalia.
Ethiopia na Somalia zilifikia makubaliano siku ya Jumatano baada ya mazungumzo ya upatanishi ya Uturuki mjini Ankara, ikiashiria mafanikio katika kutatua sintofahamu kati ya nchi hizo mbili.
Mvutano umekuwa ukiongezeka kati ya Ethiopia na Somalia baada ya Ethiopia na Somaliland kusaini makubaliano mapema mwaka huu ya kuruhusu Ethiopia kufikia Bahari ya Sham kwa kuitambua Somaliland kama taifa huru.
Somalia, ambayo inaichukulia Somaliland kuwa sehemu ya ardhi yake, ilielezea makubaliano hayo kuwa hayana nguvu za kisheria.
Kufuatia makubaliano hayo, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud walitoa taarifa ya pamoja wakisisitiza ushirikiano na mazungumzo kati ya nchi hizo mbili.
Viongozi wote wawili wamesisitiza kuheshimiana kwenye utawala, umoja, uhuru, na mamlaka ya nchi na kukubaliana kushirikiana ili kukamilisha mipango ambayo itawezesha Ethiopia kuingia na kutoka baharini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma