

Lugha Nyingine
AfDB yaongoza kukusanya fedha dola za Kimarekani bilioni 1.2 kwa ajili ya mradi wa SGR wa Tanzania
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imetoa taarifa ikisema kwamba imesaini barua ya uratibu na Benki ya Deutsche na Societe Generale ili kuanzisha mkakati wa ushirikiano wa kukusanya dola za Kimarekani bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa reli ya SGR nchini Tanzania.
Taarifa hiyo imesema makubaliano hayo, yaliyotiwa saini wakati wa Mkutano wa Uwekezaji wa Afrika mwaka 2024 huko Rabat, nchini Morocco, yanasisitiza jukumu la benki hiyo kama mratibu mkuu wa kimataifa aliyepewa mamlaka katika kuhamasisha ufadhili wa mradi huo.
Mradi huo wa SGR wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 2.3 utaunganisha bandari ya Dar es Salaam ya Tanzania katika Bahari ya Hindi na bandari ya Mwanza katika Ziwa Victoria. Kutoka Mwanza, reli hiyo ya SGR itafika hadi nchi jirani za Rwanda, Burundi, DRC na Uganda.
Hatua hiuo inaelezwa kuwa itafungua uwezo wa kiuchumi kwa kuunda njia mpya ya kupitisha bidhaa za madini na kilimo katika Afrika Mashariki na Kati.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma