

Lugha Nyingine
Rais wa DRC azindua kituo cha utamaduni kilichojengwa kwa msaada wa China
![]() |
Wageni wakiwa katika picha ya kundi kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Utamaduni na Sanaa cha Afrika ya Kati cha Kinshasha kilichojengwa kwa msaada wa China mjini Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Desemba 14, 2024. (Xinhua) |
KINSHASA - Felix Tshisekedi, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jumamosi jioni alizindua Kituo cha Utamaduni na Sanaa cha Afrika ya Kati cha Kinshasa, mji mkuu wa DRC kilichojengwa kwa msaada wa China, ambapo kwenye ziara ya kutembelea kituo hicho baada ya uzinduzi amesema "Mradi huu wa ushirikiano kati ya DRC na China unaonyesha hekima ya watu wa nchi mbili,"
"Kituo kinatarajiwa kuibua kikamilifu uwezo wa sekta ya utamaduni ya DRC huku kikiigeuza DRC kuwa kitovu cha ubunifu." Ameongeza.
Faustin Elombe, waziri wa utamaduni wa DRC, amesema kukamilika kwa mradi huo "kutaanzisha zama mpya ya uvumbuzi wa kitamaduni nchini DRC" na kuimarisha mawasiliano ya kitamaduni na uhusiano kati ya nchi za Afrika.
Elombe pia ametoa shukrani kwa China, akitoa mfano wa miradi kadhaa kati ya DRC na China, ikiwemo ile ya Ikulu ya Umma na Uwanja wa Martyrs, miradi miwili alama nchini DRC.
Marie-Therese Sombo, waziri wa elimu ya juu wa DRC, amesisitiza kuwa ushirikiano wa muda mrefu kati ya DRC na China umeipatia nchi hiyo miundombinu muhimu kwa maendeleo yake.
Kwa mujibu wa Zhao Bin, balozi wa China nchini DRC, mradi huo, alama mpya ya kipekee mjini Kinshasa, utaboresha sekta ya utamaduni ya DRC na kutumika kama jukwaa muhimu la kuonyesha utamaduni wa nchi hiyo.
Kituo hicho, ambacho jiwe lake la msingi liliwekwa na Rais Tshisekedi Mwaka 2019, kina ukumbi mkubwa wa maonyesho wenye viti 2000 na ukumbi mdogo wenye viti 800. Pia utakuwa makao ya kampasi mpya ya Taasisi ya Taifa ya Sanaa ya DRC, inayojulikana kwa mafunzo ya vizazi vya wanamuziki na wasanii wa Kongo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma