

Lugha Nyingine
Chansela wa Ujerumani Scholz apoteza kura ya kutokuwa na imani naye, na uchaguzi utafanyika kabla ya wakati uliopangwa
Picha hii iliyopigwa tarehe 16 Desemba 2024 ikionyesha Jengo la Bunge la Ujerumani, Bundestag mjini Berlin, Ujerumani. (Xinhua/Du Zheyu)
BERLIN - Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz amepoteza katika kura ya kutokuwa na imani naye kwenye Bundestag, baraza la chini la bunge la Ujerumani, siku ya Jumatatu, ambapo hatua hiyo inamaanisha kuvunjwa serikali ya mseto ya vyama vyenye wabunge wachache ya Scholz na kuanzisha mchakato wa kufanya uchaguzi wa mapema wa serikali kuu.
Kura hiyo ya kutokuwa na imani imeshuhudia wabunge 207 wakionyesha imani na Scholz, huku 394 wakipiga kura dhidi yake na 116 wakijizuia kupiga kura.
Upigaji kura wa aina hiyo haujawahi kufanyika nchini Ujerumani katika kipindi cha miongo takriban miwili.
Awali Scholz aliomba kufanya upigaji kura hiyo ya kutokuwa na imani wiki iliyopita, akitumia Kifungu cha 68 cha Sheria ya Msingi, kama njia pekee wezekana ya kuanzisha uchaguzi wa mapema. Vyama vikuu vya upinzani vimekuwa vikitoa wito wa hilo kwa muda mrefu.
Ingawa kinadharia, Scholz angeweza kuendelea kubaki madarakani bila kuwa na wabunge walio wengi, haingewezekana kisiasa kwani Bundestag isingeweza kupitisha sheria.
Wasiwasi ulikuwa umeibuka kwamba Scholz angeweza kushinda kura hiyo ya kutokuwa na imani bila kutarajia. Hali hiyo ingeweza kutokea kama wabunge wa chama cha SPD cha Scholz na kile cha Greens wangepiga kura ya kuunga mkono, huku wale wa AfD wakipiga kura kumuunga mkono ili kusababisha hali ya msukosuko.
Ili kuzuia uwezekano huo wa hali isiyotarajiwa ya wabunge 76 wa AfD kumwunga mkono Scholz ili apate kura zaidiya 367 hitajika, uongozi wa chama cha Greens uliwashauri wabunge wake kujizuia kupiga kura.
Uchaguzi mkuu wa kawaida ulikuwa umepangwa kufanyika Septemba mwaka ujao. Hata hivyo, kile kinachojulikana kama "muungano wa taa za trafiki" wa SPD, Greens, na FDP ulishindwa kuafikiana kuhusu bajeti ya pamoja ya Mwaka 2025. Hali ya kutoelewana ilijitokeza juu ya mgao wa kodi, hatua za kuhamasisha uchumi, na ukusanyaji wa uwekezaji.
Katika kilele cha mjadala huo, Chansela Scholz alimfukuza kazi Waziri wa Fedha wa FDP Christian Lindner; baadaye, mawaziri wengine wa FDP wakajiuzulu kutoka serikalini ili kujiondoa katika muungano huo unaotawala.
Baada ya kushindwa kwenye upigaji kura hiyo ya kutokuwa na imani, Scholz alienda kukutana na Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, akipendekeza kuvunja Bundestag.
Rais Steinmeier ana siku 21 za kuamua kulivunja bunge hilo. Hapo awali alisema kwamba angefanya hivyo.
Picha hii iliyopigwa tarehe 16 Desemba 2024 ikionyesha Jengo la Bunge la Ujerumani, Bundestag mjini Berlin, Ujerumani. (Xinhua/Du Zheyu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma