

Lugha Nyingine
Rais wa Eritrea asisitiza kuweka mkazo katika kuendeleza uhusiano na China
Rais wa Eritrea Isaias Afwerki amesema nchi yake inaweka mkazo mkubwa katika kukuza uhusiano kati yake na China.
Rais Isaias amesema hayo wakati akipokea hati ya utambulisho ya Balozi wa China nchini Eritrea Bw. Li Xiang katika mji mkuu wa nchi hiyo, Asmara, akisisitiza kuwa, nchi yake inapenda kudumisha mabadilishano ya ngazi ya juu na China na kufanya mawasiliano na uratibu wa mara kwa mara.
Kwa upande wake Balozi Li amesema, China iko tayari kushirikiana na Eritrea kutekeleza vizuri makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili na matokeo yaliyopatikana katika Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Beijing, kuimarisha kuaminiana kisiasa kati ya nchi hizo, kuendeleza ushirikiano wa kivitendo, na kuimarisha urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma