

Lugha Nyingine
Afisa wa Umoja wa Mataifa asema Afrika inatazamia nishati ya nyuklia kwa mustakabali endelevu
Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA) Claver Gatete amesema, Afrika inahitaji nishati ya nyuklia kwa ajili ya maendeleo endelevu.
Akizungumza katika mkutano wa ngazi ya mawaziri wenye kaulimbiu “Kufadhili Nishati ya Nyuklia barani Afrika kwa Siku Zijazo” uliofanyika katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, Jumatatu wiki hii, Bw. Gatete amezungumzia nafasi ya Afrika kama kiongozi wa dunia katika uzalishaji wa urani, huku Namibia na Niger zikiwa katika nafasi tano za mwanzo za wachangiaji wakuu.
Kwa mujibu wa Bw. Gatete, Bara la Afrika linaendelea kuwa eneo la mwisho duniani kwa usambazaji umeme, huku karibu watu milioni 600 wakikosa ufikiaji wa huduma ya umeme wakati huo huo nishati ya nyuklia ikiwa na uwezo wa kuwa chanzo cha mabadiliko kwa uhamaji wa Afrika kwenda nishati mbadala.
Naye Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Jimmy Gasore, amesisitiza haja ya uratibu kati ya wadau ili kukabiliana na changamoto ya nishati barani Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma