DRC yaishutumu kampuni ya Apple kwa kutumia madini yanayopatika kwenye migogoro

(CRI Online) Desemba 19, 2024

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imewasilisha malalamiko ya uhalifu nchini Ufaransa na Ubelgiji dhidi ya kampuni tanzu za kampuni ya Apple, ikiituhumu kampuni hiyo kwa kutumia madini yanayotoka kwenye maeneo yenye migogoro.

Mawakili wa DRC wamedai kuwa kampuni ya Apple inashiriki kwenye uhalifu unaofanywa na makundi yenye silaha ambayo yanadhibiti baadhi ya maeneo ya migodi mashariki mwa DRC.

Mamlaka nchini Ufaransa na Ubelgiji zimesema zitaangalia kama kuna ushahidi wa kutosha kuchukua hatua za kisheria zaidi, lakini kampuni ya Apple imepinga vikali madai hayo, ikisema iko makini sana katika kutafuta uwajibikaji kwenye mambo ya madini.

Mawakili wa DRC wamesema kuna mnyororo wa ugavi wa Apple kuchafuliwa na "madini ya damu" wakitaja madini ya bati, tantalum na tungsten wanayodai kuwa yamechukuliwa kutoka maeneo yenye migogoro na "kusafishwa kupitia minyororo ya kimataifa ya ugavi".

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha