Umoja wa Mataifa watoa wito wa ulinzi wa watoto wahamiaji barani Afrika

(CRI Online) Desemba 19, 2024

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa wito wa ulinzi zaidi kwa watoto wahamiaji katika kanda ya Afrika kusini mwa Sahara kutokana na kuongezeka kwa matishio ya maisha na hadhi zao.

Katika taarifa yao ya pamoja iliyotolewa jana jijini Nairobi, Kenya, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) pamoja na shirika la hisani la Save the Children yamesema, Afrika ina idadi kubwa zaidi ya watoto wahamiaji kutokana na migogoro, umasikini na dharura zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Mashirika hayo yamesema, watoto barani Afrika wanaokimbilia maeneo ya Ghuba, Ulaya na Kusini mwa Afrika wanakabiliwa na hatari za vurugu na kudhalilishwa, huku wengi wakishikiliwa na wengine kuuzwa na kutumikishwa kwa lazima.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha