

Lugha Nyingine
NATO yasema nchi wanachama wake hazilazimiki kusaini mkataba wa usalama na Ukraine
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO) Mark Rutte ambaye yupo ziarani nchini Bulgaria amesema nchi wanachama wa Jumuiya hiyo hazilazimiki kusaini mkataba wa pande mbili kuhusu usalama na Ukraine.
Rutte alisema hayo alipokutana na wanahabari akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Bulgaria ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Atanas Zapryanov.
Rutte amesema baadhi ya nchi wanachama wa NATO zimefikia makubaliano husika na Ukraine na nyingine bado zinaendelea na mazungumzo, lakini jambo muhimu zaidi ni kuhakikisha pande zinazohusika zinapata msaada wa kijeshi.
Pia ameongeza kuwa hivi sasa nchi wanachama zinakabiliwa na upungufu wa bajeti ya serikali, na kutoa wito kwa nchi hizo kuhakikisha matumizi ya ulinzi na kuongeza uwekezaji katika sekta hiyo ili kuhakikisha viwanda vinavyohusu mambo ya ulinzi vinazalisha kwa wingi zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma