

Lugha Nyingine
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aitaka Israel kuacha kukiuka mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya Syria
(CRI Online) Desemba 20, 2024
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameitaka Israel kuacha kukiuka mamlaka ya Syria na ukamilifu wa ardhi yake.
Akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari, Bw. Guterres amelaani mashambulizi makubwa ya Israel ya kupiga mabomu kutoka angani dhidi ya Syria yenye lengo la kuharibu silaha za kimkakati na miundombinu ya kijeshi, na kuingiza wanajeshi wake katika eneo lisilo la kijeshi kati ya Syria na Mlima Golan inayokaliwa na Israel.
Bw. Guterres amesisitiza kuwa Israel na Syria lazima zitekeleze masharti ya Mkataba wa Kuondoa Majeshi wa mwaka 1974, ambao bado unatumika kikamilifu.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma