Wapalestina 20 wauawa katika shambulio la mbomu lililofanywa na Isael mjini Gaza

(CRI Online) Desemba 20, 2024

Wapalestina 20 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa katika mashambulio ya mabomu yaliyofanywa na Israel na kulenga shule mbili zinazohifadhi watu waliokimbia makazi yao na nyumba moja mashariki mwa Mji wa Gaza.

Vyanzo vya habari vya huko na mashuhuda wamesema, ndege ya Israel ilifanya mashambulio ya kupiga mabomu kutoka angani dhidi ya shule za Al-Karama na Sha’ban Al-Rayes ambazo zilikuwa zinatumika kuwahifadhi raia waliokimbia makazi yao, na pia nyumba moja iliyoko Al-Tuffah mashariki mwa Mji wa Gaza.

Msemaji wa Idara ya Ulinzi wa Raia ya Palestina, Mohamoud Basal ameliambia Shirika la habari la China Xinhua kuwa, timu za uokoaji na wafanyakazi wa afya wamepata miili 20 kutoka eneo lililoshambuliwa kwa bomu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha