

Lugha Nyingine
Idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga Chido nchini Msumbiji yafikia 73
(CRI Online) Desemba 20, 2024
Shirika la Kudhibiti Hatari na Kupunguza Maafa la Msumbiji jana limesema, idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga Chido nchini humo imeongezeka hadi 73, na watu wengine 543 wamejeruhiwa.
Kimbunga hicho kiliyakumba majimbo ya Cabo Delgado na Nampula, na kusababisha uharibifu mkubwa, na kuwalazimisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao na miundombinu muhimu iliharibiwa.
Serikali ya Msumbiji imefungua vituo viwili vya hifadhi vya dharura, ambavyo kwa sasa vinawahifadhi watu 1,349 wanaohitaji msaada wa haraka.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma