Namibia yatenga megawati 330 za umeme wa jua kuboresha usalama wa nishati

(CRI Online) Desemba 20, 2024

Namibia imetenga megawati 330 za uwezo wa nishati ya jua kwa uwakala na utekelezaji kama sehemu ya mpango wake wa ngazi ya mawaziri wa mwaka 2024.

Waziri wa Madini na Nishati wa nchi hiyo Tom Alweendo amesema jana kwenye taarifa yake, kwamba uwezo huo mpya utagawanywa kati ya kampuni ya nishati ya serikali NamPower na wazalishaji binafsi wa nishati.

Amesema mpango huo unaakisi mkakati wa kina unaoendana na malengo mapana ya kiuchumi na ahadi ya serikali ya nchi hiyo chini ya makubaliano ya kimataifa kuhusu mazingira.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, NamPower itashughulikia maendeleo ya miradi mingine mingi ya umeme wa jua, ikiwemo Kituo cha kuzalisha umeme wa jua cha Rosh Pinah ambacho kitaongeza uzalishaji wake kwa megawazi 30 zaidi, na kufanya uwezo wake wa jumla kufikia megawati 100.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha