

Lugha Nyingine
Semina ya kwanza ya mafunzo ya kilimo cha msaada wa China yafanyika nchini DRC
Waziri wa Kilimo wa DRC Gregoire Mutshail Mutomb (katikati) akijulishwa kuhusu mradi wa ushirikiano wa kilimo katika Kituo cha vielelezo vya teknolojia za kilimo na Uenezi wa Mimea inayokukua kwa kutegemea mvua cha Kinshasa, DRC. (Picha na Shi Yu/Xinhua)
Semina ya kwanza ya ushirikiano wa teknolojia za kilimo inayoandaliwa pamoja na China na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeanzishwa tarehe 19 huko Kinshasa.
Waziri wa Kilimo wa DRC Gregoire Mutshail Mutomb alitoa hotuba kwenye ufunguzi wa semina hiyo, akisema kuwa, kilimo ni moja kati ya nguzo za ushirikiano kati ya DRC na China, ambazo ziliinua ngazi ya uhusiano wao kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote mwezi Mei mwaka jana.
Waziri Mutomb alisema, mafunzo hayo ya kwanza yatafanya DRC iweze kutumia vizuri rasilimali zake za kilimo, kutimiza lengo la kujitosheleza katika uzalishaji wa chakula na kupunguza umaskini.
Balozi wa China nchini DRC Zhao Bin alitoa wito wa kufanya juhudi za pamoja za nchi hizo mbili, ili kupanua ushirkiano wao wa kilimo na kusaidia DRC kuimarisha usalama wa chakula.
Semina hiyo itafanyika kwa mwezi mzima, na wanafunzi zaidi ya 40 wa DRC watashiriki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma