

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akagua vikosi vya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) vya Macao
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), katika ziara yake akikagua vikosi vya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao, kusini mwa China, Desemba 20, 2024. (Xinhua/Li Genge)
MACAO - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) siku ya Ijumaa alikagua vikosi vya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao baada ya kuhudhuria mkutano wa hadhara wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 tangu Macao kurudi katika nchi ya China.
Alasiri ya Ijumaa iliyopita, Rais Xi alikagua vikosi vya jeshi na kukutana na wajumbe wa maofisa na askari wa vikosi vya jeshi huko Macao.
Amesisitiza kuwa ni lazima kuongeza uwezo wa ulinzi wa jeshi kwa pande zote na kuchangia zaidi katika kufanikisha mambo mapya ya uzoefu wa "nchi moja, mifumo miwili" kwa umaalum wa Macao.
“Katika miaka 25 iliyopita, vikosi vya jeshi vilivyoko Macao vimetekeleza jukumu muhimu katika kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya taifa, na kufanya kazi muhimu kwa ajili ya ustawi na utulivu wa muda mrefu wa Macao,” Rais Xi ameeleza.
Rais Xi amesisitiza ni lazima kushikilia bila kuyumba uongozi kamili wa Chama juu ya jeshi, kufanya juhudi za kuimarisha kwa pande zote kazi ya kujenga jeshi kwa nidhamu kali na kudumisha viwango vya juu vya umoja, usalama na utulivu katika vikosi vya jeshi.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikutana na wajumbe wa maofisa na askari wa vikosi vya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) vilivyoko katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao, kusini mwa China, Desemba 20, 2024. (Xinhua/Li Gang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma