Wabunge wa China wasikiliza ripoti kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 23, 2024

Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC) akihudhuria mkutano wa pili wa wajumbe wote wa kamati ya kudumu ya 13 ya bunge hilo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 22, 2024. (Xinhua/Li Tao)

Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC) akihudhuria mkutano wa pili wa wajumbe wote wa kamati ya kudumu ya 13 ya bunge hilo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 22, 2024. (Xinhua/Li Tao)

BEIJING - Wabunge wa China wamekutana jana Jumapili kujadili na kupitisha ripoti kwenye mkutano unaoendelea wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC) ambapo Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya bunge hilo, alihudhuria kikao cha wajumbe wote wa mkutano huo.

Mkutano huo umesikiliza ripoti ya utekelezaji wa Sheria ya Mali Zinazomilikiwa na Serikali kwenye Kampuni. Ripoti hiyo imependekeza kuanzisha na kuboresha mfumokazi wa wakala wenye mamlaka ya kusimamia mashirika yanayomilikiwa na serikali na mtaji wa serikali.

Wabunge pia wamepitia ripoti ya utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Mto Manjano, ambayo inataka kuhimiza usimamizi unaozingatia sheria hiyo na kuendeleza uhifadhi na urejeshaji wa mfumo wa ikolojia kwenye bonde lake.

Pia wamesikiliza ripoti ya marekebisho ya makosa ya ukaguzi wa mahesabu ya serikali mwaka 2023, ambayo imesema kuwa hadi mwishoni mwa Septemba, mchakato wa kurekebisha makosa hayo ulihusisha fedha za yuan jumla ya bilioni 538 (dola za Kimarekani kama bilioni 74.8), wakati huohuo zaidi ya watu 2,800 walikuwa wamewajibishwa.

Mkutano huo pia umejadili ripoti ya ugawaji na matumizi ya fedha za bajeti kwa ajili ya kuzuia na kupunguza athari za maafa, na kukabiliana na dharura. Ripoti hiyo imependekeza kuboresha sera na mifumo ya bajeti, na kuboresha miundo ya ugawaji wa fedha.

Mkutano huo pia umesikiliza ripoti za ulinzi wa mashamba, kumbukumbu na mapitio ya sheria, na kushughulikia utovu wa nidhamu na ufisadi uliotokea miongoni mwa watu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha