

Lugha Nyingine
Uturuki na uongozi mpya wa Syria zadhamiria kuimarisha uhusiano baada ya mazungumzo
(CRI Online) Desemba 23, 2024
Kamanda wa kundi la HTS (Hayat Tahrir al-Sham) Ahmed al-Sharaa na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan ambaye yuko ziarani nchini Syria, wamefanya mazungumzo jana Jumapili na kudhamiria kuimarisha uhusiano kati ya pande hizo mbili.
Akiongea katika mkutano na wanahabari uliofanyika baada ya mazungumzo yao, Bw. Fidan ameeleza matumaini yake kwa "mustakabali mzuri zaidi" wa Syria na pia ameahidi kuwa Uturuki itaiunga mkono Syria katika kujenga upya miundombinu, kukarabati taasisi na kurejesha Wasyria waliokimbia mgogoro.
Kwa upande wake, Bw. al-Sharaa ameitaja Uturuki kama “rafiki kwa watu wa Syria”, akisema pande hizo mbili zinalenga kujenga uhusiano wa kimkakati unaonufaisha mustakbali wa eneo hilo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma