Watu 11 wafariki katika ajali ya basi kaskazini magharibi mwa Tanzania

(CRI Online) Desemba 23, 2024

Ajali ya basi la abiria kugongana na gari jingine katika wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, imetokea siku ya Jumamosi kaskazini-magharibi mwa Tanzania kutokana na hitilafu ya breki na kusababisha vifo vya watu 11 na wengine 16 kujeruhiwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Blasius Chatanda amesema breki ya basi hilo ilikuwa na tatizo kwenye eneo korofi, na kusababisha basi hilo kurudi nyuma na kugongana na gari lililokuwa limesimama.

Ajali hiyo ilitokea saa 8 mchana katika eneo la msitu wa Kasibdaga, na baada ya kugongana na gari hilo lililokuwa limesimama basi hilo lilitumbukia kwenye korongo, kupinduka na kung'olewa sehemu yake ya juu lakini viti vyote vilibaki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha