

Lugha Nyingine
Burhan wa Sudan atoa wito kwa Umoja wa Mataifa kukomesha kuingiza silaha Darfur
Abdel Fattah Al-Burhan (kulia) mwenyekiti wa Kamati ya Mamlaka ya Mpito ya Sudan ambaye pia ni kamanda mkuu wa Jeshi la Sudan (SAF) akipeana mkono na Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Ramtane Lamamra kwenye mkutano wao katika mji wa Port Sudan, Jimbo la Bahari Nyekundu, mashariki mwa Sudan, tarehe 23 Desemba 2024. (Baraza la Mamlaka ya Mpito ya Sudani/kupitia Xinhua)
KHARTOUM - Mwenyekiti wa Kamati ya Mamlaka ya Mpito ya Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan, ametoa wito wa kutaka Umoja wa Mataifa (UN) kuchukua hatua ili kuhakikisha utekelezaji wa maazimio ya Baraza la Usalama ya kukomesha kuingizwa kwa silaha katika eneo la Darfur magharibi mwa Sudan na kuzuia mashambulizi dhidi ya mji wa El Fasher.
Kamati ya mamlaka ya mpito imesema katika taarifa yake kuwa, amrijeshi mkuu wa Jeshi la Sudan (SAF) Bw. Burhan ametoa wito huo jana Jumatatu alipokutana na Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Ramtane Lamamra katika mji wa mashariki wa Port Sudan.
Al-Burhan amesisitiza dhamira ya Sudan ya kufanya juhudi pamoja na Umoja wa Mataifa katika kuweka matarajio ya pamoja ya kazi ya baadaye katika sekta zote, pamoja na kulinda raia, akitoa wito wa kutaka Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa kuweka shinikizo kwa wanamgambo wa Vikosi vya Uungaji Mkono wa Haraka (RSF) na kulaani vitendeo vyake vya mashambulizi.
Mjumbe huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari kuwa mkutano huo umejadili hali ya Sudan.
"Wakati wa mkutano huo, nilithibitisha kuwa Umoja wa Mataifa unajihusisha na kuhimiza kufanya mazungumzo ili kutatua msukosuko wa Sudan," Lamamra amesema.
Mjumbe huyo ameeleza kuwa vita hivyo vilivyodumu kwa miaka takriban miwili vimesababisha waathirika wengi, Umoja wa Mataifa na mashirka yake yako tayari wakati wote kushirikiana zaidi na Sudan ili kutatua msukosuko huo wa Sudan na kukomesha mateso ya watu wa Sudan.
Juni 13, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuitaka RSF isitishe kuzingira El Fasher, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini. RSF imekuwa ikiizingira El Fasher tangu Mei 10.
Septemba 11, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa kauli moja azimio la kuongeza muda wa vikwazo dhidi ya Sudan -- ikiwa ni pamoja na kuzuia mali, marufuku ya kusafiri, na vikwazo vya silaha -- hadi Septemba 12, 2025.
Sudan imekuwa katika mgogoro mbaya kati ya SAF na RSF tangu katikati ya Aprili 2023.
Mashirika ya kimataifa yametoa makadirio mapya yakisema kuwa, mgogoro huo mbaya umesababisha vifo vya watu zaidi 28,700 na kusababisha watu wengine milioni 14 kuwa wakimbizi, ama ndani au nje ya Sudan.
Abdel Fattah Al-Burhan (kulia) mwenyekiti wa Kamati ya Mamlaka ya Mpito ya Sudan ambaye pia ni amrijeshi mkuu wa Jeshi la Sudan (SAF) alikuwa na mazungimzo na Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Ramtane Lamamra kwenye mkutano wao katika mji wa Port Sudan, Jimbo la Bahari Nyekundu, mashariki mwa Sudan, tarehe 23 Desemba 2024. (Kamati ya Mamlaka ya Mpito ya Sudani/ kupitia Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma