Ukame uliosababishwa na El Nino waathiri msimu wa kilimo Kusini mwa Afrika

(CRI Online) Desemba 24, 2024

Wakulima wa eneo la kusini mwa Afrika wanaendelea kukumbwa na changamoto kutokana na hali ya El Nino kuleta madhara kwa msimu wa kilimo wa 2024/2025.

Baadhi ya wakulima wa Afrika Kusini wameathiriwa zaidi, huku wengine athari hizo mbaya za El Nino zikiwa zimeharibu asilimia 70 ya mazao yao.

Kutokana na kipindi kirefu cha ukame, eneo la Kusini mwa Afrika limekumbwa na ukame mkali zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, huku mvua ikifikia asilimia 20 tu ya viwango vya kawaida.

Mchumi mkuu wa Shirikisho la Biashara ya Kilimo la Afrika Kusini Bw. Wandile Sihlobo, amesema uzalishaji wa mahindi wa Afrika Kusini ulikuwa chini zaidi ya asilimia 22 kwa mwaka, wakati Zambia na Zimbabwe zilipoteza nusu ya mazao yao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha