Uganda yazindua viwanda vinane vyenye thamani ya mamilioni ya dola vilivyowekezwa kwa mtaji kutoka China mwaka 2024

(CRI Online) Desemba 24, 2024

Waziri wa Uganda anayeshughulikia mambo ya biashara, viwanda na ushirika Bw. David Bahati amesema Uganda imezindua viwanda vinane vyenye thamani ya mamilioni ya dola za kimarekani vilivyowekezwa kwa mtaji kutoka China, ambavyo vimetoa fursa za ajira za moja kwa moja kwa maelfu ya watu wa Uganda.

Bw. Bahati ameeleza kuwa kati ya viwanda hivyo, vinne vilizinduliwa na Rais Yoweri Museveni, kikiwemo Unisteel, kiwanda kipya cha chuma, ambacho kina uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 100 na kuajiri watu zaidi ya mia tano.

Waziri huyo amesema sekta ya viwanda ya Uganda inachangia asilimia 27.4 katika Pato la Taifa (GDP) la nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha