

Lugha Nyingine
Thamani ya shilingi ya Kenya yaimarika kabla ya msimu wa sikukuu
Benki Kuu ya Kenya (CBK) imesema shilingi ya Kenya imepata nguvu dhidi ya dola ya Marekani na kuuzwa kwa shilingi 129.29 kabla ya msimu wa sikukuu ya Krismasi.
Thamani ya shilingi ya Kenya ilishuka kwa pointi 130 dhidi ya dola ya Marekani mwanzoni mwa mwezi Desemba wakati ilipokuwa ikikabiliana na shinikizo la sarafu za kimataifa.
Benki kuu imesema hali hiyo ya kuimarika kwa sasa inachangiwa na kupungua kwa mahitaji ya dola na kupanda kwa akiba ya fedha kabla ya sikukuu.
Hadi sasa thamani ya shilingi ya Kenya imeongezeka kwa asilimia 17.6 mwaka hadi mwaka dhidi ya dola ya kimarekani, ikiwa ni tofauti na kushuka kwa asilimia 26.8 kipindi kama hicho mwaka 2023.
Hata hivyo inakadiriwa kuwa shilingi ya Kenya bado itaendelea kukabiliwa na shinikizo mwaka 2025.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma