

Lugha Nyingine
Shughuli ya Uenezi Duniani ya Mtandao wa Vituo vya “Dhahabu” wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ya 2024 Yaanzishwa Yiwu
Ili kusoma zaidi na kutekeleza mawazo muhimu ya Katibu Mkuu Xi Jinping kuhusu ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, hususan hotuba yake muhimu katika kongamano la nne la kazi ya ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, shughuli ya uenezi duniani wa mtandao wa vituo vya “dhahabu” wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”ya 2024 ilianzishwa katika mji wa Yiwu, mkoa wa Zhejiang, Desemba 22.
Niu Yibing, naibu mkuu wa Ofisi ya Kamati Kuu ya Mambo ya Mtandao wa Intaneti ya China ambaye pia ni naibu mkuu wa Ofisi ya kitaifa ya Mambo ya Mtandao wa Intaneti ya China, na Zhao Cheng, mjumbe wa kudumu wa Kamati ya Chama ya Mkoa wa Zhejiang ambaye pia ni mkuu wa Ofisi ya Uenezi ya Mkoa wa Zhejiang walishiriki kwenye shughuli hiyo.
Shughuli hiyo itatumia jukwaa la mtandao kuonyesha kikamilifu utafutaji wa uvumbuzi na matokeo dhahiri ya Mkoa wa Zhejiang katika ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kuonyesha dunia dhamira na vitendo vya China vya kuhimiza kujenga Jumuiya ya binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja katika zama mpya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma