Ripoti ya mfanyakazi mpya | Mfanyakazi wa Tanzania: Anajionea utengenezaji wa ala za muziki za kimagharibi huko Wuqiang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 25, 2024

Aris anayetoka Tanzania anaishi hapa China na anapenda muziki sana. Wakati akijua Mji wa Wuqiang wa Mkoa wa Hebei ulioko kaskazini mwa China ni “mji wa ala za muziki”, ambao pia ni kituo cha kutengeneza ala za muziki, aliamua kuutembelea mji huo kujionea ufundi wa kazi ya mikono ya utengenezaji wa ala za muziki.

Katika Kampuni ya Jinyin ya Wuqiang, fundi Li Shiqi mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika sekta hiyo, alimwongoza Aris kutembelea kwenye kiwanda cha kampuni hiyo, ambapo walichunguza mchakato wa utengenezaji wa ala nyingi za kimagharibi. Hata Aris alipata nafasi ya kujifunza jinsi ya kucheza tarumbeta! Akiwa "mfanyakazi" mpya kabisa wa kampuni, Aris alionyesha fahari kubwa, akisema "Muziki hauna mipaka, ndoto hazina kikomo!"

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha