

Lugha Nyingine
Wizara ya Fedha ya China yasema kuongeza matumizi ya fedha mwaka 2025
Picha hii iliyopigwa tarehe 12, Agosti imeonesha majengo marefu kwenye Eneo la Kiini la Biashara la Beijing, China. (Picha na Li Xin/Xinhua)
Wizara ya Fedha ya China imeahidi kuongeza matumizi ya fedha na utoaji wa dhamana za kiserikali mwaka 2025, ili kutoa uungaji mkono wenye nguvu zaidi kwa kuhimiza utulivu wa ukuaji wa uchumi.
Kwenye mkutano wa kitaifa wa kazi za fedha uliofanyika kwa siku mbili na kumalizika jana Jumanne, Lan Fo'an, Waziri wa Fedha wa China alisema kuwa, China itatekeleza sera kuhusu matumizi ya fedha za kuchochea hamasa zaidi mwakani, ili kuhakikisha sera za matumizi ya fedha zinadumisha nguvu yake na ufanisi wake.
Msimamo wa sera hiyo inaendana na misingi ya mkutano wa kazi za uchumi wa Kamati Kuu ya Chama , uliofanyika hivi karibuni. Katika mkutano huo, watungaji wa sera wameamua kutekeleza sera za fedha “zinazolegea kwa kiasi kinachofaa” mwaka 2025, ambazo ni tofauti zaidi na sera "tulivu" zilizotekelezwa katika miaka 14 iliyopita.
Hivi sasa China inaharakisha kukabiliana na changamoto za uchumi za ndani na nje ya nchi, ili kudumisha ufufukaji tulivu wa hatua madhubuti wa uchumi
Lan alisema, China itaweka uwiano wa nakisi ulio wa juu zaidi, kuongeza matumizi ya fedha , kuhakikisha fedha zinapangwa kwa haraka zaidi, kuboresha muundo wa matumizi ya fedha , kuweka mkazo zaidi katika kuboresha maisha ya watu, kuhimiza matumizi na kudumisha mwelekeo wa ongezeko la uchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma