Nchi tisa zikiwemo Indonesia na Uganda Zawa nchi washirika wa BRICS

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 25, 2024

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning alipojibu swali kuhusu orodha ya nchi washirika wa BRICS iliyotangazwa na Rassia tarehe 24 Desemba alisema kuwa familia kubwa ya nchi za BRICS imekaribisha nchi washirika wapya, hii imeonesha ushirikiano kati ya nchi za BRICS umeendelea kwenye ngazi mpya. China ingependa kushirikiana na nchi wanachama na nchi washirika wa BRICS katika kuhimiza maendeleo ya sifa bora ya “Ushirikiano Mkubwa wa BRICS”.

“Oktoba mwaka huu, Rais Xi Jinping alihudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS uliofanyika Kazan na kufikia makubaliano muhimu na viongozi wengine wa nchi za BRICS kuhusu kuongeza nchi washirika wa BRICS. Hii ni hatua nyingine muhimu katika maendeleo ya BRICS baada ya upanuzi wa kihistoria wa mwaka jana”. Mao Ning alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari wa kawaida kwamba, baada ya mkutano wa Kazan, China ilishirikiana na nchi mwenyekiti Russia na wanachama wengine wa BRICS katika kuhimiza kazi ya kuongeza nchi washirika. Hatimaye, nchi tisa ziliamuliwa kuwa nchi washirika wa BRICS: Indonesia, Malaysia, Thailand, Belarus, Bolivia, Cuba, Kazakhstan, Uzbekistan, na Uganda.

(Gazeti la People’s Daily)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha