

Lugha Nyingine
WFP kusambaza majiko 5,000 ya kupikia kwa jumuiya za wakimbizi wa Tanzania
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeanza maandalizi ya kusambaza majiko 5,000 ya kupikia yanayotumia nishati kidogo kwa jumuiya zinazohifadhi wakimbizi wa Tanzania katika mkoa wa Kigoma.
WFP imesema katika taarifa yake kuwa usambazaji wa majiko hayo una lengo la kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa, kuboresha ufanisi wa nishati, na kupunguza matatizo ya rasilimali za ndani karibu na kambi za wakimbizi.
Taarifa imesema ugawaji wa majiko hayo ni kazi inayoratibiwa na kwa ushirikiano na Kituo cha Kitaifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni Tanzania na OffgridSun, kampuni ya Italia iliyobobea kwenye teknolojia ya matumizi ya nishati ya Jua kwenye mikoa isiyofikiwa vya kutosha na umeme wa gridi ya taifa.
Mwezi Mei Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alizindua mkakati wa taifa wa dola bilioni 1.8 za Marekani, ili kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma