

Lugha Nyingine
Katika Mkuu wa UM aonesha wasiwasi kuhusu msukosuko wa njaa nchini Sudan
(CRI Online) Desemba 25, 2024
Msemaji wa Umoja wa Mataifa ametoa taarifa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesikitishwa na hali ya usalama wa chakula inayozidi kuwa mbaya nchini Sudan, na kutoa wito kwa pande husika kutoa msaada wa kibinadamu.
Taarifa imesema baada ya miezi zaidi 20 ya vita, watu milioni 24.6, ikiwa ni zaidi ya nusu ya watu wa Sudan, wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Taarifa hiyo imesema Umoja wa Mataifa na washirika wake wanaongeza msaada wa chakula na misaada mingine muhimu kwa watu walio hatarini zaidi, lakini mapigano yanayoendelea na vizuizi dhidi ya usafirishaji wa misaada na wafanyakazi, vinaendelea kuhatarisha operesheni za utoaji wa msaada.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma