

Lugha Nyingine
Barabara mbili zilizopitika kwa miaka 70 zashuhudia maendeleo ya kiajabu ya “Paa la Dunia”
Picha iliyopigwa tarehe 28, Julai, 2023 ikionesha swala wa Kitibeti wakivuka barabara ya Qinghai-Xizang na kuelekea eneo la chanzo cha mito mitatu mkoani Qinghai. (Zhang Hhongxiang/Xinhua)
Tarehe 25, Desemba, 2024 ilikuwa ni Siku ya miaka 70 tangu barabara za Sichuan-Xizang na Qinghai-Xizang zilipoanza kupitika kwa magari. Wastani wa mwinuko wa eneo zima la Barabara ya Qinghai-Xizang ni wa mita 4,000 kutoka usawa wa bahari, na eneo zima la barabara ya Sichuan-Xizang linajulikana kama "Maonesho ya Maafa ya Kijiolojia", ambapo halijoto ya chini na upungufu wa oksijeni ni changamoto za kila dakika kwa uwezo wa uvumilivu wa binadamu. Katika miaka 70 iliyopita, wafanyakazi zaidi ya 100,000 wa ujenzi wa barabara walikwenda kwenye eneo hilo la Uwanda wa Juu wa Qinghai-Xizang, kujenga barabara na madaraja, wakifanya miujiza ya maendeleo ya kiajabu ya uwanda huo wa juu ambao unajulikana kuwa "Paa la Dunia".
Tarehe 25, Desemba, 1954, barabara hizo mbili zenye urefu wa jumla wa zaidi ya kilomita 4,300 zilianza kupitika kwa pamoja kwa magari ya kwenda Lhasa, zikikomesha hali ya Xizang ya kutofikika kwa barabara.
Tarehe 11, Januari, 1955, hafla ya kupitika kwa magari kwenye Barabara za Kangzang (kwa sasa inaitwa barabara ya Sichuan-Xizang) na Qinghai-Xizang ilifanyika huko Lhasa. (Picha na Liu Shilin, Ren Yongzhao/Xinhua)
Kuanzia barabara hizo mbili, mtandao wa barabara kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Xizang umeendelea sana, na mawasiliano ya usafiri umekuwa rahisi zaidi. Hivi sasa urefu wa jumla wa barabara zilizojengwa katika mikoa ya Xizang na Qinghai umefikia kilomita 212,700. Miji yote ya wilaya kwenye "Paa la Dunia" imefikiwa na barabara.
“Zamani ilichukua wiki nzima kwa kufika huko, lakini sasa kufika huko kunahitaji siku mbili tu,” alisema Ma Fujun, dereva wa kusafirisha mizigo kwa muda mrefu kwenye barabara ya Qinghai-Xizang.
Tarehe 1, Julai, 2006, ujenzi wa reli ya Qinghai-Xizang kwenye eneo lenye mwinuko zaidi kutoka usawa wa bahari duniani, reli hiyo ambayo ni yenye urefu zaidi inayopita sehemu kubwa zaidi za ardhi inayoganda, ulikamilika na kuanza kupitika kwa magari. Katika miaka minne iliyopita, reli ya Sichuan-Xizang ilianza kujengwa, ikiwa reli nyingine ya kuelekea Uwanda wa Juu wa theluji.
Tangu ilipoanzisha rasmi usafiri wa ndege mwezi Machi, 1965, mpaka sasa Xizang kwa jumla imekuwa na njia 180 za usafiri wa ndege. Kufunga safari kutoka Lhasa kunaweza kufika sehemu mbalimbali nchini China ndani ya siku moja tu.
Hivi sasa kwenye kando za barabara za Sichuan-Xizang na Qinghai-Xizang, watu wa makabila mbalimbali wamejenga na kuendesha vituo vya kutoa vitu vya mahitaji, wakihudumia wasafiri wa kuja na kuondoka.
Picha iliyopigwa tarehe 11, Julai ikionesha Daraja kubwa lenye njia mbili la Mto Yarlung Tsangpo kwenye Bonde la Zangmu lenye urefu wa mita 525.1, na tao lake kuu lina upana wa mita 430. (Picha na Liu Hongming/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma