

Lugha Nyingine
China na Japan zafikia makubaliano kuhusu mawasiliano ya kitamaduni kati ya watu wao
Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi, na waziri wa mambo ya nje wa Japan Bw. Takeshi Iwaya, wamehudhuria mkutano wa pili wa utaratibu wa ngazi ya juu wa mashauriano kuhusu mawasiliano ya watu kati ya China na Japan katika sekta ya utamaduni, yaliyofanyika Jumatano mjini Beijing.
Pande mbili zimefikia makubaliano kumi, ikiwa ni pamoja na kuhimiza mawasiliano na safari za masomo kati ya vijana wa nchi hizo mbili, ushirikiano katika sekta ya elimu, ushirikiano katika shughuli za utalii, na ushirikiano kwenye mambo ya miji rafiki.
Pande mbili pia zimesema zitaimarisha ushirikiano kwenye sekta ya michezo, ushirikiano katika tasnia za utamaduni na burudani, ushirikiano kwenye sekta ya habari na jumuiya za washauri bingwa, mambo ya wanawake, kujenga kwa pamoja maonesho ya Expo ya Osaka ya mwaka 2025, na kuandaa mkutano wa tatu wa ngazi ya juu wa mawasiliano kati ya China na Japan.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma