

Lugha Nyingine
China yatuma shehena mbili za msaada wa dharura wa ubinadamu kwa Gaza kupitia Misri
Ubalozi wa China nchini Misri, umesaini makubaliano na Palestina kutuma shehena mbili za msaada wa dharura wa kibinadamu kwa Ukanda wa Gaza.
Hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, ilifanyika Jumatatu huko Cairo, balozi wa China nchini Misri Bw. Liao Liqiang na balozi wa Palestina nchini Misri Bw. Diab al-Louh walishiriki kwenye hafla hiyo.
Balozi Liao amesema ili kupunguza hali ngumu ya ubinadamu katika Ukanda wa Gaza, serikali ya China imeendelea kutoa msaada kwa Palestina akiongeza kuwa China imewasilisha shehena nyingi za msaada, ikiwa ni pamoja na chakula na dawa kwenye eneo hilo kwa kupitia Misri.
Amesisitiza kuwa China iko tayari kudumisha mawasiliano na uratibu wa karibu na Palestina na Misri, ili kutoa msaada zaidi kwa eneo la Gaza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma