

Lugha Nyingine
Shambulizi la kuvizia lasababisha vifo vya maofisa 14 wa serikali ya mpito ya Syria katika jimbo la Tartus
Waziri wa mambo ya ndani ya serikali ya mpito ya Syria Mohammed Abdul Rahman amesema maofisa 14 wa serikali ya mpito wameuawa huku wengine 10 wakijeruhiwa katika shambulizi la kuvizia lililotokea Jumatano wiki hii katika jimbo la Tartus Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Akinukuliwa na gazeti la kienyeji la Al-Watan, waziri huyo amewataja washambulizi wa tukio hilo kuwa ni wa nguvu iliyobaki ya serikali ya zamani. Maofisa hao waliuawa wakati walipokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kudumisha usalama na kuwalinda raia.
Habari zinasema mivutano ya kimadhehebu imeongezeka nchini Syria baada ya serikali ya Bashar al-Assad kupinduliwa, na maofisa wa usalama wameonya kuwa nguvu zilizobaki za serikali ya zamani zinaweza kutumia migogoro kati ya madhehebu kuzusha mifarakano.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma